UBEPARI NA MAENDELEO YA VITU
Mara nyingi watu tumeshindwa kutofautisha maendeleo ya vitu na watu. Tunapoona barabara nzuri tunaona tuna maendeleo japokuwa wanafunzi wengi waliomaliza vyuo vikuu nchini hawana kazi! Tunapoona majumba mazuri na marefu tunaona maendeleo japokuwa hosipitali hazina madawa na bei ya madawa machache iko juu! Tunapoona tuna Channel nyingi za TV na Bongo Flavas kwa wingi tunahisi tuna maendeleo wakati mikakati ya kupambana na rushwa imejaa rushwa!!!!!!!!!
